TAASISI YA TAALUMA ZA
KISWAHILI
UFADHAILI WA MASOMO YA MA KISWAHILI
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni
ya ALAF Limited inafuraha kuwatangazia ufadhili wa ada kwa wanafunzi watatu (3) wa kusoma Programu ya M.A Kiswahili katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam kwa mwaka wa masomo 2019/2020.
Mwaombaji awe na sifa zifuatazo:
1. Raia wa Tanzania
2. Mhitimu wa BA Kiswahili
3. Awe na wakia (GPA) usiopungua 3.8 wa Digrii ya Kwanza
4. Awe amepata Udahili wa M.A Kiswahili CKD
5. Umri usiozidi miaka 25
6. Awe ni muhitaji wa udhamini
7. Awe na uwezo wa kujigharimia mahitaji mengine (chakula, steshenari,
malazi, utafiti n.k)
Nyaraka Muhimu za Kutuma
1.
Barua ya maombi ambayo pia itabainisha uwezo
wako wa kitaalumma
2.
Nakala ya cheti cha Matokeo ya Kitaaluma ya
Shahada ya kwanza (Transcript)
3.
Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
4.
Maelezo mafupi (Ukurasa mmoja) kueleza kwa nini unahitaji
huo ufadhili
Maombi yatumwe kwa:
Ofisi ya Mkurugenzi,
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Jengo la Kiswahili, Ofisi Na. 209 AU
Email: iks@udsm.ac.tz
Tangazo hili linatangazwa kwa mara ya pili
Maombi yatapokelewa kuanzia:
Tarehe 6 Novemba 2019 Mpaka
Tarehe 11 Novemba 2019
Watakaofanikiwa watajulishwa tarehe 13 Novemba 2019


0 comments:
Post a Comment