SIMULIZI FUPI

Labels:



Ilikuwa ni siku ya Furaha kwa David coz wazazi wake walikuwa wanaenda UK and yeye na mdogo wake wa kike Dalvina walikuwa Holiday kwani Chuo chao walikuwa wamefunga and baba yao aliwaacha na magari kibao pia mpunga wa kutosha  so David akaona hiyo ndo chance ya yeye Kufurahi, Alipotoka tu Airport akawapigia simu washkaji zake waende zao kujirusha wakaenda zao sea clif nyumbani akimuacha mdogo wake peke yake. Mdogo wake nae akaona ampigie simu mpenzi wake aje home. Dalvina Akujua kuwa anakamilisha misheni ya John aliyetumwa kuja kulocate familia yake na kuwaua. 
Baada ya bata ndefu David  anarudi home anakuta nyumba iko shagala bagala na mdogo wake wa Dalvina hayupo pia anaona kama kuna sign ya damu hivi , anazidi kupatwa na wasi wasi ukizingatia anampenda sana mdogo wake na wazazi wake walimkabidhi yeye alinde nyumba na mdogo wake pia but badala yake yeye akaenda kulewa na rafiki zake. Anazunguka kila chumba na kuita kwa sauti kubwa lakini hamkuti mdogo wake machozi yanaanza kumtoka anarudi sebuleni anakuta Tv inaonyesha habari kuwa ndege moja kutoka Tanzania, ikimilikiwa na British Airways imeanguka na kuua watu wote waliokuwemo machozi yanazidi kumtoka huku akilia kwa sauti ya uchungu kwani wazazi wake walikuemo kwenye ile ndege ghafla anaskia sauti ya gari kwa nnje anaona watu wakiwa wamevalia nguo nyeusi wakiwa wameshika mapanga bila kufikiria David anakimbia kupitia mlango wa nyumba na anafungua geti la nyumba na kutoweka.
Alienda coco beach mida ya saa nane za usiku alikaa peke yake machozi yakimtoka na asijue la kufanya kwanza hakujua ni akina nani wale na je wale ni watu waliomchukua mdogo wake na je wazazi wake walikufa kifo cha kawaida au waliuliwa, alipanga kesho yake aende polisi kutoa Taarifa kuwa mdogo wake ametekwa,
Kesho yake anaenda oystarbay kuripoti tukio anafika pale anamkuta askari wa zamu anamwambia kila kitu but askai anamuuliza we ndo David anamwambia ndio je, baba yako ndo aliyekufa kwenye ajali ya ndege David anajibu ndio.Askari anamwambia subiri kidogo hapo diishani alafu anaingia ndani mara moja David taratibu ananyata hadi mlangoni anasikiliza nini kinaendelea anasikia askari akisema Yule nyie wapumbavu mnafanyaje kazi Yule kijana yupo hapa polisi niko nae hapa si mlisema mmewaua wote kwa mbali anaskia askari akisema fanya haraka uje kumalizia kazi yako hapa mi ntamuweka mpaka uje .
Erick anashinkwa na tumbo la ghafla machozi yanamlenga na haja kubwa inambana ghafla huku jasho likimtoka kama maji, anarudi dirishani(reception) haraka na Yule askari anakuja anamkuta David jasho likimtoka na anamuuliza we vipi mbona jasho ivo david anamji bu Kichwa kinauma sana naomba kwenda toilet mara  moja askari anamuelekeza toilet na David anakwenda huko na ananawa uso na anapanga amtoke Yule askari anaruka ukuta na kutokea upande wa pili anakimbia hadi morocco. Anahema sana alikaa chini muda mrefu asijue la kufanya maana kila alichofanya hakuna wa kumsaidia na kila mtu alikuwa anaitaka roho yake.
Erick anaamua kwenda bank kwenda kutoa hata pesa kidogo aende zake iringa kwa bibi yake and anaingia bank kila mtu anamshangaa maana alikuwa mchafu na hajaoga toka usiku, anajaza karatasi anakwenda dirishani but anaambiwa hawezi kutoa pesa maana acaunti yake imefungwa labda akamuone manager, anaenda hadi kwa meneja , meneja anashangaa sana kwani yeye alichojua David pamoja na familia yake wote wamekufa laini hakuonesha mshangao wake hadharani maana hakutaka David hajue. 
Anamwambia baba yako kabla hajasafiri yeye na mwanasheria wake walikuja na kufunga Ac kwani hawakukuambia niligoma na kumwambia hakuna kitu kama hicho Ac ilkuwa chini ya jina langu na yeye hata kama alinifungulia hana mamlaka ya kufunga ile AC bali ni mimi mwenyewe. Ananiambia atashughulikia suala langu niondoke nije kesho nagoma kuondoka na kuanzia bonge la varangati polisi wanakuja wanantoa na kuntupa nnje, naamuakwenda kwa mwanasheria wa baba nafika tu      nakuta anakaribia kufa najitahidi kumsaidia midamu ilijaa kila kona ya mwili wangu nashtusha na sauti za watu wakiniambia uko chini ya ulinzi. Nikafungwa pinga na kupelekwa polisi Oysterbay.
MAelezo..
Askari..inasemekani mali zote zilikuwa chini ya baba yako mdogo nda maana ukaamua kumuua mwanasheria wa baba yako na ujaribu kuchukua mali za baba yako.
Mimi.kichwani (kumbe baba mdogo nae anahusiku) nikamjibu Yule askari sijui anachokizungumza na ni haki ya kila mwanachi kupatiwa mwanasheria kwa hiyo siongei chochote mpaka nipatiwe mwanasheria. Narudihwa rumande nikisubilia mwanasheria nitakaye pewa maana sikuwa na uwezo wa kumlipia wa binafsi ikabidi nisubili ntakaye pewa na serikali.
Kesho mwanasheria anakuja na naanza kuongea nae kitu cha kwanza ananiuliza je umemuua kweli? Nakataa kwani ndi ukwelu huo nashangazwa na mwanasheria akiniambia nikubali tu kuwa mimi ndie niliefanya kwani watu wanaohusika na hilo swala ni wakubwa sana na kamwe siwezi kuwashinda na watanifata popote nilipo na kuniaua so nikubali tu nipewe pesa nikaishi zangu UK,nilikataa katu katu na kumfukuza kama mwizi.
Dalvina......anashtuka katika usingizi na kumkuta mpenzi wake akiwa nae but wakiwa sehemu ambayo haifahami cha kwanza anauliza kama yangu yupo wapi anamjibu sijui alipo kwani hapa tupo wapi lover wake anamwambia tuko mahali salama Dalvina anaanza kulia na kumwambia mpenzi siamini kama wewe umenifanyia hivi mimi nakupenda kwa dhati kumbe mwenzangu una mambo yako, James alimbembeleza pasi na mafanikio kasha akamwambia ukweli wote kuhusu yeye kuwa wale jamaa walikuwa na mama yake na wakamwambia asipofanya vile wangemuua mama yake na pia aliambiwa amuue Dalvina but yeye aliwasaliti na kutorka nae baada ya mama yake kuachiwa. Dalvina anamwambia James kama kweli anampenda ampeleke kwa kaka yake, James anamwambia hajui alipo na hana uhakika kama yuo hai maana kuna watu walitumwa wakamuue.
David anafikiria sana na anaamua kutoroka na anapanga bonge la mpango anamuita mwanasheria wake na kumwambia wakienda mahakamani wiki inayokuja anakiri mambo yote alofanya lakini anahitaji kitu kimoja tu,wamfungulie AC yenye Milion mia na pia wamuonyeshe kabla hajaenda mahakamani mwanasheria akamuambia sawa na baada ya siku mbili anaonyesha kila document yake anamwambia akazipost kwenye po box Fulani hivi.
Siku ya siku inafika anapelekwa kwa basi la wafungwa hadi mahakami kisutu mwanasheria anajua kazi ni raisi sana na inafika zamu ya David kuhulizwa but kabla hajaulizwa anaanza kulalamika tumbo linamuuma anapelekwa haraka muhimbili kufika huko anawapiga askari wote na kuwatoroka anaenda posta haraka anachukua document zake zote na kutoa pesa kama shilingi million moja kwenye ATM na kwenda zake huko kibaha kwenye nyumba ya baba yake ya siri.
Dalvina..
Baada ya dalvina kuongea sana James anakubali kumsaidia kipenzi chake kumtafuta kaka yake but kwanza Dalvina anamwambia waende kibaha kwenye nyumba ya siri ya baba yake. Wakakae huko maana huko ndo salama bila kujua kuwa James alichokuwa anasubilia ndo icho waende tu kwenye hiyo nyumba ya siri akafanye yake.
David
Kwa mbali kwenye security camera anawaona James na Dalvina anafurai sana na kukimbia kuwafungulia Dalvina anamkumbatia kaka yake kwa furaha but anageuka anashangaa James akiwa ameshika Bastola akiwaamuru wakae chini, James haraka anaenda kwenye computer ya Yule Jamaa ana erase kila kitu na kufanikiwa kutoa siri zote ambazo baba yake James alikuwa nazo dhidi ya kundi kubwa la kigaidi lililokuwa limeanzisha na mzee khamis.
Na kuondoka zake kwa kasi ya ajabu Dalvina analia sana kwani mwanaume aliyemuamini sana ndie aliyemsaliti bu baada ya tukio lile David anaanza kujiuliza kumbe varangati lote lile lilikuwa ni kuhusu zile data lakini David anakumbuka kuwa baba yake alimpa Memory card flani hivi na akawa ameiweka kwenye chain yake anaamua kuitoa na kuangalia nini kilichomo anakutana na mikataba mikubwa ya nchi na watu waliosaini mikataba kinyume na sheria pia anakutana na kila kitu kuhusu wake magaidi. Anaapa atafanya kila awezalo awaangamize wale magaidi.
Dalvina anambembeleza sana kaka yake bila mafanikio mweishowe anaamua kumwacha tu maana hata yeye alitaka awaone mbele ya sheria.
Anaanza taratibu kuwaangamiza, anaingia kwenue vitu vya baba ake anakuta bastola ba kupanga kuua mmoja baada ya mwingine alafu mwishoni atajisalimisha,anaanza kumsaka James kwa udi na uvumba anafanikiwa kujua alipo anapanga usiku wake amvamie na akamuue lakini kabla anamuambia mdogo wake aenda kwa bibi yake moshi kwanza na mdogo wake anakubali anaondoka asubui yake.
Anawai katika nyumba ya james mapema kabla hajarudi na kujificha ndani, James anarudi akiwa amechoka anafungua mlango na kuingia ndani anatulia zake kwenye kochi na anawasha TV anaanza kuangalia Habari lakini ghafla anashtushwa na mtu akitokea jikoni kwake anakimbilia bastola yake lakini eick anamwambia unatafuta hii sasa kaa hapo chini fanya haraka  sijaja kukutania mimi hapa James kwa uoga anasema nsamehee David amamuuliza kosa lako ni nini anasema kila kitu na James anamrekodi na kusepa zake. David alituma Hile sauti ya James akisema kila alilofanya na aliyemtuma kwa mwanadada mmoja Detective sarah.  Sarah aligraduate katika chuo cha police moshi na ilikuwa ni kaze yake ya kwanza ya mauaji alipewa jukumu la kusimamia kesi  ya James hadi ampate muuaji, anaenda eneo la tukio anaangalia sana but bado hapati pa kuanzia.
Anarudi nyumbani akiwa amechoka sana anakuta kitu mlangoni kwake anachukua anafungua na kukutana na voice ecorder anasikiliza mwanzo mwisho na kujua kuwa Aliyekuwa akongea ni James aliye uwawa basi moja kwa moja akawa anajua aliyemrecord ndie aliyemuua James so akaanza kumsaka David kwa udi na uvumba. Kumbuka James aliacha na namba yake ya simu ili Yule dada awasiliane nae pindi atakapopata ile recorder dada anampigia James na James anamwambia unatakiwa uje peke yako sehemu nitakayochagua mimi na nitakapogundu aumekuja na mtu ntakuua sarah akakubali. Kuna baadhi ya maafisa waliokuwa wanamsaka David walipopata ile habari wakaona ule ndo muda wa kwenda kumuua David, sarah anaambia aende manzese darajani anafika pale anakutana na dogo anamuambia twende wanatembea sana kasha Yule dogo anamwambia lete simu yako anaitupa na kukutana na dogo mwingine tena anampeleka sehemu anamwambia subiri hapo linakuja gari fasta anaambia panda haraka david alikuwa akiendesha tunaenda hadi maeneo ya kimara kasha tunaanza kuongea namwambia kila kitu but sarah anaonekana kama haamini hivi na alikuwa ameficha bastola yake anaitoa na kumwambia uko chini ya ulinzi. Kabla hajamaliza kuongea million ya bunduki inasikika walikuwa ni polisi wakijaribu kumuua David sarah anawaambia jaman acheni nimeshamkamata  lakini  hawajali kasha David anamkamata sarah na kumuonyesha bastola akisema ntamuua anapanda nae gari na kuondoka kwa kasi njiani anamwambia unaona hivi ndivo wanavyofanya mipango yao by killing people and nakuhakikishia wakati naondoka nilimuacha James mzima na sijui aliyemuua labda umtafute maana ndo kazi yako hiyo but mimi kazi yake ni kuwapeleka mbele ya haki wote waliohusika na kuisambaratisha familia yangu.
Tulifika sehemu tuliongea sana na Sarah akahaidi kunsaidia mwanzo mwisho , anapiga simu kwa mkubwa wake anamuamini sana na kumweleza kila kitu na mkubwa wake anahaidi kunsaidia kusafisha jina langu na kusema kesho tu atafungua kesi lakini nahitajika kutoa ushaidi nkasema hilo so tatizo kwangu.
Kesi inafunguliwa na ushaidi wote ninao mimi wanaohusika wote wanapelekwa mahakamani , nafisha sehemu moja ya siri sana sije wakaniua kwa ushaidi niliokuwa nao, lakini wale watu hawakuacha kunsaka kwa udi na uvumba. Mwishowe wanatumwa kuja kulipua sehemu ambayo nimefichwa ili kupoteza ushaidi na siku ya kesho ndo ilikuwa siku ya mwisho ya kesi ambayo mimi nilitakiwa kutoa ushaidi wangu.
Niliamua kutoroka siku moja kabla ya kesi ya mwisho na nikaenda zangu disco na Sarah na sarah akaniahidi kunrudisha mapema tulikaa sana disco ilipofika saa nane usiku tukaamua kurudi but tunafika karibu na nyumba tunakuta nyumba ikiteketea kwa moto Sarah na mimi wote tulikuw tumezima simu so mkuu wa polisi alipagawa mara kwa mbali namuona mkuu tunamfuata na anashngaa sana na kuuliza mmeponaje afu mnanuka pombe, Sarah ulienda wap na shahidi lakini kwa kuwa kitendo ulichofanya kimemuokoa shaidi ntakuacha kwa leo lakini inatubidi tutoe taaifa kuwa wewe na huyu shaidi mmekufa wote ili wale watu waamini ivo tunakubaliana na taarifa inatolewa pale kuwa tumekufa kwenye mlipuko but mkuu anatuma taarifa mahakamani kuwa kesi iendelee kama kawaida.
Kesho asubuhi na mapema tunajiandaa lakini hatuingii kortini kwanza kwa mbali tunaskia wakili wa wale jamaa akisema kama hakuna ushaidi wa kutosha naomba kesi ifungwe na pia mimi na mteja wangu tutafungua kesi ya madai dhidi ya serikali kwa kutudhalilisha hivi,. Natokeza na kusema nanni kasema ushaidi hakuna naanza kwa mbwebwe pale ndugu hakimu nilichoshika mkononi ni memory kadi yenye kila madudu waliofanya hawa jamaa pia nina sauti ya mtu waliyemtuma kuangamiza familia yangu akikiri mwenyewe pia kuna baadhi ya askari walikuwa wakisaidiana nao nina ushaidi wa kutosha wa picha na video kila kitu baba yangu alikuwa anakifanyia kazi ndo maana wakaamua kumuua baba yangu kisa huu ushaidi , mh hakimu tunayemuona pale ni kiongozi wa kkundi cha kigaidi kilichoanzishwa mwa........... na walipanga kuja kuipindua serikali ya Tanzania lakini baada ya baba kuwagundua ndo wakaamua kufanya huo uamuzi na hawa jamaa wamejaa kila kona nawajua kwa majina na picha zao ninazo nawapa kila ushaidi pale na hakimu anatoa uamuzi wa kila anaehisika akamatwe wote wanakamatwa na kila mmoja anahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

0 comments: