SEASON PREMIERE
STORY BY En drizzi Tunechi
...................................................
MREMBO BONGO FLAVOR
WRITTER: EN DRIZZY TUNECHI (ERICK NZIKU)
STORY BY: EN DRIZZY TUNECHI (ERICK NZIKU)
CAST: BONGO ARTIST
EPISODE: 1
Aliazaliwa miaka ya themanini katika kijiji kimoja huko songea, aliishi katika mazingira magumu sana na akiwa na umri mdogo tabia yake ilianza kujionyesha kwanza hakuwa mtu anayependa shule pia alikuwa anapenda kushinda vijiweni na watoto wa kiume ,sura yake na umbo lake viliwavutia wengi lakini hawakumuelewa mpaka miaka ya tisini ndo watu walianza kumuelewa na kumpenda ..
Jina lake anaitwa Irene makuya lakini wengi wanapenda kumuita mrembo kutokana na uzuri wake usio na kipimo, ana macho nyororo na kiuno cha dondora pia kifuani saa sita ukimuona we mwenyewe utadata. Huyu demu bila nigga j mpaka leo hakuna ambaye angemfahamu, jamaa alimtoa ushamba wake wa kijijini na kumuingiza katika jiji la Bongo, alimpa umaarufu pia na mwanaume wa kwanza kuonja penzi lake .
Nigga j bwana alidata sana na penzi lake hadi dar es salaam nzima ikajua kama nigga j anatembea na Irene,kadri umaarufu ulivozidi huyu demu jina lake watu wakaanza kulisahau na kwa kuwa alikuwa kaiteka bongo watu wakawa wanamuita MREMBO WA BONGO katika jijini la dar es salaam ndo alizaliwa upya tena.Mrembo wa bongo halikuwa hakatai kila haliyejaribu alimpa penzi na kila alieonja alitamani flava yake na hakuna alieacha kusimulia kama mrembo wa bongo ana flava tofauti tofauti na ukimpata utatamani uonje flava zote. Jina lake likazidi kubadilika watu wakawa wanamuita mrembo wa bongo mwenye flava lakini kuna jamaa akatokea anaitwa JOHN DILUNGA akampa jina kwa ufupi na kumuita BONGO FLAVA,
Tokea hapo umaarufu wake uliongeza maradufu na wasanii wengi wakaanza kumpenda pia walikuwamo wasanii wa kike sister p na zay b na Lady jayde , Sister p na Zay b waligombana sana kisa mrembo bongoflava hadi wakawa wanarushiana maneno kwenye nyimbo zao kisa huyu demu.
Radi nazo hazikuwa nyuma katika kusambaza umaarufu wa bongo flava haswa radio one kila mda walikuwa wanalitaja jina la huyu demu.hadi ikafikia baadhi ya wasanii kumtungia nyimbo kwa majina tofauti tofauti.
Mchizi dully sykes alituona sie maboya eti akampa jina lingine hili atuzuge lakini hakuna aliyeshindwa kutambua kwamba Dully alizimika kwa mrembo bongo na kumbatiza jina la jullietta , alimtungia hadi kanyimbo kanaenda hivi
“julietta nakupenda kwa dhati ,
Lakini majirani wanachombeza unafiki
Naapia aki ya mungu sikuachi,
Penzi letu litazidi kupanda kwenye chati”
Hayo ndo yalikuwa maneno ya Dully kwa mrembo bongo flava.
Mrembo bongo alivutia wanaume wengi sana hadi wakawa wanamuimbia pia kina dada wenzake pia hawakusita kumpa sifa zake kipindi kile cha Zayb na sister waligombana sana kisa huyuhuyu bongo flava.kila mmoja alikuwa anajiona bora mbele ya bongo flava zayb alikuwa na mashairi yamejaa visado na sister alikuwa anamtisha kila siku kwamba anakuja …
Fuatilia story hii ya mrembo wa bongo
Na ujue
- Jinsi mrembo atakavopoteza umaarufu na kutembea na watoto
- Watu wanavopoteza uhai wao katika harakai hii ya kuwa na bongoflava
- Watu wanavopata umaarufu kupitia huyu mrembo
- Jinsi mchizi hiphop alivokuja kugombana nae
- Jinsi mashauzi yalivoshusha umaarufu wake
- Namengine mengi


hiyo gud