STORY "SIKU 14 ZA KARANTINI NA MUME WA MTU"

Labels:

Ilikua siku ya jumatatu asubuhi napokea simu kutoka uhamiaji wakinifahamisha kua passport yangu iko tayar.ilikua siku ya furaha sana kwangu kwani nilikua nahamu na safari ya kwenda italy ikiwa ndo mara yangu ya kwanza katika maisha yangu i was so happy that sikulala iyo siku hadi naamka asubuhi nawaza kwenda kuchukua passport yangu.
Siku ilikua njema nimetoka kitandani mapema sikuwa na uchovu pamoja na kutolala usiku kucha nikajiandaaa na kwenda zangu posta wizara ya mambo ya ndani kufata pasport yangu,nilifanikiwa kupata pasport yangu na kuipeleka moja kwa moja ofisini kwaa jili ya kuandaa ticket za ndege kwa aajili ya safari yetu kikazi tulikua wasichana wawili na mwanaume mmoja yani mimi elizabeth , cesilia na jimmy.
Siku ya siku ikawadia safarai ikaaanza kuelekea italy kwa ndege ya alfajiri kupitia dubai. Ilikua safari ndefu lakini sikua na uchovu sababu ya hamu ya kufika italy kwa mara ya kwanza tuliingia central station airport asubuhi ya saa tatu katika jiji la milan kila saa sikuacha kupiga picha sura yangu ilikua ya tabasamu zito ikipambwa na furaha ya kufika millan kwa mara ya kwanza.
Safari yetu ikaishia katika hotel moja ya kifahari ndani ya jiji la milan hotel da vinci bonge moja ya hotel ikigharimu taribani laki nne kwa usiku mmoja hakika safari yetu ilikua njema. Siku ya kwanza millan tulitembelea kanisa la Santa Maria delle Grazie ambalo inaaminika kuna picha ya last super iliyochorwa na kijana mashuhuri leonardo da vinci pia tulitembelea mall kubwa ya Galleria Vittorio Emanuele bila kusahau tulienda makumbusho ya Teatro alla Scala tulirud tukiwa tumechoka so tukala na kwensa kulala huku kesho yake ikiwa ni siku ya seminar iliyotuleta.
Nikiwa italy tunaskia dunia inapata mshtuko baada ya kukubwa na gonjwa la ajabu covid-19 lakini hakuna aliejali akidhani ni ugonjwa wa china pekee bila kujua ni ugonjwa hatari na unaosambaaa haraka sana. Kila mtu ndani ya millan alikua busy sana hakuna aliejali kama kuna ugonjwa umekuja kazi zilikua zinaendelea kama kawaida na china alijaribu kuionya dunia lakini hakuna aliejali kama kawaida tukafanya seminar siku ya kwanza na kumaliza.
Siku moja kabla ya kuondoka italy tulipelekwa kuangalia mechi ya uefa kati ya atalanta na valencia ilikua mara yangu ya kwanza kuingia uwanjani nilifurai sana kuwa mmoja ya watu walioshuhudia mchezo ule.
Siku ya siku ikawadia safari ya kurudi tanzania ikawadia na kama kawadia tukaanza safari ya kuja tanzania kupitia dubai, tukiwa kwenye ndege naskia watu takribani elfu arobaini walioshuhudia mechi kati ya atalanta na valencia wamehathirika na corona mwili uliingia kibaridi ghafla na mawazo yakaanza kuntawala lakini sikujali sana maneno yaliyokua yanasemwa kua mtu mweusi hapati corona yalinupa faraja.
Tukaingia alfajiri tanzania nikashtushwa na kauli ya maofisa wa pale wakisema wasafiri wote inabidi muingie karantini kwa siku 14 kwa gharama zenu wenyewe ilikia habari mbaya sana kwangu lakini pia ilikua lazima upimwe joto mimi pamoja na wenzangu tukapimwa na kukutwa tuko sawa lakini ilibidi tikae karantini siku 14 kabla hatujaruhusiwa Kuingia uraiani.
Kwa kua hatukua na pesa kwani tulitumia zote kufanya shopping italy ikatubidi tukae chumba kimoja watu watatu lakini haikupita siku maofisa walikuja na kumchukua cesilia kwa iyo nikabaki mimi na jimmy tu ndani ya chumba kimoja .

STORY YETU NDO INAANZIA HAPO SHARE STORY HII YA KWELI NA KUSISIMUA NEXT WEEK JUMATATU SEHEMU YA PILI INAKUJA

0 comments: