Writer: Storikka
Genre: historical.
Short story: Lupembe ni Mji wa kubuni tu na matukio yote ya kubuni lakini yakiaangazia ukweli wa hali halisi ya Tanganyika kabla na wakati wa uhuru.
SEHEMU YA KWANZA
Giza nene alafu kuna watu wawili walikuwa wakinifukuza kwa mbali nawaona wamevaa nguo nyeupe huku wakiwa wameshika vitu mkononi sikuwa na muda wakuvitizama sana kwani nilishawajua ni wale waarab sisi tulikuwa tukiwaita waadhabu kwa mateso waliyokuwa wakitupa, nilikimbia sana tena sana nilianguka nikasimama na kuendekea kukimbia , hadi nikafika karibu na kwenye kambi yetu kambi ya Lupembe na kutaka kuingia haraka ndani kwani hapo ni salama maana hakuna mwarabu yeyote aliyediriki kugusa kambi ya Lupembe.
Giza nene alafu kuna watu wawili walikuwa wakinifukuza kwa mbali nawaona wamevaa nguo nyeupe huku wakiwa wameshika vitu mkononi sikuwa na muda wakuvitizama sana kwani nilishawajua ni wale waarab sisi tulikuwa tukiwaita waadhabu kwa mateso waliyokuwa wakitupa, nilikimbia sana tena sana nilianguka nikasimama na kuendekea kukimbia , hadi nikafika karibu na kwenye kambi yetu kambi ya Lupembe na kutaka kuingia haraka ndani kwani hapo ni salama maana hakuna mwarabu yeyote aliyediriki kugusa kambi ya Lupembe.
Kambi ya Lupembe ilikuwa mkoani Iringa sasa Njombe milimani huko hakuna mtu aliyeweza kuisogelea maana tulikuwa tunasifika kwa vita za mawe na maji ya moto, mimi mandonda ni mzaliwa wa lupembe nikiwa mtoto pekee wa mzee ng’ande ambaye alichukuliwa na waarabu kama mtumwa, Maisha ni ya raha sana katika ngome yetu tukiongozwa na Lupembe Mzenge, Lupembe ana watoto wawili mmoja wa kike na mmoja wa kiume wa kike Aisha na wa kiume Kondo.
Kondo alisifika kama shujaa wa kijiji chetu hakuna vita aliyekwenda na kurudi bila mafanikio watu walimuogopa sana na kumtukuza kama Mungu, alisifika pia kwa Tabia yake ya kupenda wasichana na kukataa wapenzi wa dada ake Aisha kila aliyetaka kumuoa Aisha alimkataa na kusema hakidhi vigezo vya kumuoa Dada ake so Bado alikuwa Akimsaka shujaa ambaye atamuoa Dada ake.
Kabla sijaingia katika Ngome kwa nikamuona Msichana akiwa anakuja huku anakimbia kwa mbali tena nikamuona mtu akiwa anamkimbiza moja moja nikajua mwarabu fasta nkachomoa upinde wangu na mshale na kumlenga Yule mtu nilipoachia tu moja moja ukamkuta Yule jamaa na kuanguka hapo hapo, Yule msichana alipofika nilishangaa kumuona mtoto wa mfalme Aisha akaniambia naomba usimwambie kaka maana ataniua nikamjibu asihofu maana si nafasi yangu kumwambia, Tulipiga story sana na Aisha mwishowe akarudi ndani na mimi nikarudi ndani nikaenda zangu kulala,
Baada kama ya masaa manne hivi nikaanza kusikia kelele za watu wakilia bila kusimama nikaamua kutoka nilipotoka nilipigwa na butwaa kuona kila kona ikiwaka moto watu wakiwa wamekufa huku waarabu wakishangilia fasta akili yangu ikamkubuka Aisha mtoto wa Mfalme nikamfuata haraka na kukuta yuko salama nikamchukua na kuanza nae safari ya kutoroka nilijua kila kona ya lupembe na kila njia ya kutorokea tukiwa tunatoroka kwa mbali nilimuona Lupembe akiwa amekufa na mwanaye Kondo akiwa chini ya ulinzi wa waarab, Aisha alikuwa akilia sana lakini nikamshika kwa nguvu na kuondoka nae, tunatokeza kwa ile njia ya kutorokea nikakutana na kundi la watu wakiwa na hasira wakiwa wameshika mpanga na mishale wakisema tunamtaka Aisha huyo ni halali yetu lazima afe leo
SEHEMU YA PILI
Sikuwa tayari kumuona Aisha akifa mbele ya macho yangu so kwa kuwa wale jamaa walikuwa wakiniamini sana nikawaomba tumfunge kwanza Aisha atuambie kilichotokea na tujue kwanza maadui zetu wanataka nini ndo tumuue waligoma sana mwishowe wakakubali tukaenda hadi kwenye kambi ndogo ya Lupembe tulizoea kuiita retreat zone ngome iyo ilijengwa kwa msaada wa mcdonald Cameroon kutoka Great Britain so yeye ndo aliipa jina kwa Heshima yake. Aisha alifungwa kwa one of the holding cell ikabidi niende kujua why Aisha did what she did aliniambia mwanzo mwisho kuwa waarabu wako na mama yake ambaye alikuwa aiishi ndani ya ngome ya Lupembe so hakuwa na Jinsi Zaidi ya kutusaliti nkamuahidi Aisha Hatokufa na mama Yake ntamsaidia atampata ile nageuka tu nataka niondoke nikapigwa na kitu kizito kuamka nikajikuta tupo mimi na Aisha na wale jamaa zetu wakiwa wametuzunguka tayari kwa kutuua kwa kututupa kwenye shimo la mateso mzungu aliipa jina la snake hole maana kuna nyoka zaidi ya mia moja kila aina ya nyoka,
Mimi na Aisha kwa pamoja tukatupwa kwenye lile shimo Aisha alikuwa akilia sana hadi machozi yakamkauka mimi nilikuwa nikimuomba mungu tu anisaidie niweze kuepuka dhaama iliyoko mbele yangu ghafla nyoka wengi wakatuzunguka nyoka mmoja likuwa mkubwa sana akasimama mbele na ghafla akageuka na kuwa mwanamke mmoja mzee, tulitetemeka sana mimi na Aisha ghafla akaanza kuongea kwa sauti ya mikwaruzo Mandonda tumekuchagua kuwa kiongozi na shujaa wa Lupembe hakuna utakachoshindwa katika maisha yako , mara nyoka wote wakapotea ukaja mwanga na kutuonyesha sehemu ya kutokea kwa uoga tuliufuata ule mwanga na kutokea shemu moja nzuri sana karibia na mto ruaha moyoni nkasema this is the place where new Lupende will be established najisemea ivo wakati nikijua dhairi kuwa kitu kama icho ni ndoto , ndoto ambaye si raisi kutimiza, tulikaa siku tatu polini na kuamua kurudi katika retreat zone tulipofika watu walishangaa sana maana hakuna aliyewahi kupona lile shimo na snake na badala yake walitupa heshima kubwa na kusema watatusaidia katika kila jambo.
Mipango ya kwenda kumuokoa mama yake Aisha ilianza lakini ilibidi kwanza tujikamilishe kijeshi ndo twende tulifanya mafunzo ya kurusha mmikuki na mishale usiku kucha hadi nilipoona kuwa wameiva...
Asubui yake tukajiimu mapema tayri kwenda kumuokoa mama yake Aisha, Aisha alikuwa kiongozi maana yeye ndiye aliyekuwa akipajua mama yake alipo tulitembea sana mwishowe tukafika sehemu na Aisha akasema tushakaribia tupite ivi alafu baada ya dk 10 tutakuwa tumeshafika wanaume tukajiandaa tukawa tayri kwa lolote lakini baada kama ya hatua kumi hivi nikashangaa watu wakianza kuzama chini robo tatu ya watu nlokuwa nao walizama chini kwenye shimo na kwa mbali tukaanza kupigwa na risasi cha kushangaza nageuka nyuma simuoni Aisha , sikuwa tena na nguvu za kupambana ikabidi niwaambie tukimbieni jamani. Nilikimbia huku nikiwanatoa machozi sikuamini kama Aisha ametuingiza kwenye mtego tena nilijisemea labda kuna kitu bado sikuwa tayari kuamini
Itaendelea, je undhani Aisha anafanya kazi na waarabu kutuangamiza au?
FOLLOW THIS LINK KWA GROUP YA HABARI
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/I9bqBYpASOiCrFrEmivwyl
FOLLOW THIS LINK KWA GROUP YA HABARI
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/I9bqBYpASOiCrFrEmivwyl


0 comments:
Post a Comment