I GOT LUCKY

Labels:

KILA MTU ANA JINSI YAKE YA KUELEZE JINSI ANAVYOMPENDA MTU LAKINI HUYU MREMBO NI HATARI SANA!......KAA NA MIMI NIKUPE FULL MKANDA...............
One day katika mishe zangu maeneo ya tegeta nkamuona mrembo mmoja mkali sana na kilichonifanya nimuangalie zaidi ni kwamba nilimuona Ubungo lakini sikumfuatilia sana sababu unajua duniani hapa kila mtu ana mishe zake..
Nafika eneo nililikuwa nawkenda ambapo ni kiwanda cha wazo hill namkuta yule demu nnje akiongea na mshua mmoja hivi wa kizungu bado sikuwa na mawazo yoyte na yeye nkaingia ndani kufuatilia barua yangu ya field but nashangaa kufika tu naambiwa we ndo erick nkasema ndio tumeamua kukuajiri kutokana na vigezo vyako but m nkawaambia mi bado nasoma chuo wakasema usijari tunalijua hilo na utapewa muda wa kusoma usijari.Natoka nnje nakutana na mchizi mmoja jinsi anavyoonekana anaonekana kama dereva wa lile gari na si mwenye gari ananiuliza si unaenda kimara nkasema ndio twenzetu mi naelekea hukohuko but tunafika kimara ananishusha nashangaa anageuza na kurudi zake....

Nafika home nashangaa napokelewa vizuri na mama mwenye nyumba nkakuta amepika chakula kizuri akanipa na wakati kila siku zilikuwa kelele za kodi na akaniambia nisiwe na shaka naweza kukaa kwenye nyumba yake hadi nitakavyo nilishangaa sana but nkawa kimya tu ikanibidi niingie room kwangu kuingia tu simu inaita napokea na kuweka sikioni dah nakutana na sauti tamu sana yenye kubembeleza ikisema pole na uchovu kisha akakata, nILIpigwa na butwaa ikabidi niipige ile namba kwa kivocha changu cha ngama but haikupokelewa na kupiga tena ikawa haipatikani nkapotezea ikanbidi nilale zangu.

Usiku ulikuwa mrefu kichwani nikimwaza yule demu niliyemnuona mara tatu sura yake umbo lake ilikuwa taswira nzuri sana mbele ya macho yanu niliisi namtizama bado, usingizi ukanchukua nikalala naamka asubui nachukua simu nicheki time nakutana na message ikisema "wear black trou and white shirt" dah nkasema nini hii nkapiga ile namba haipatikani nkaenda zangu kuoga narudi nafungua kabati nivae sioni nguo zangu hata moja nguo zote ni mpya na nakutana na black trou na white shirt zikiwa zimenyooshwa vizuri dah ikanbidi nivae tu lakini kichwani nikawa nawaza ni nani huyu anaenifanyia mambo yote haya,sipati jibu....
Natoka zangu nnje nkapande daladala nakutana na ile gari ya jana jamaa akisema njoo nkupe lift nkasita kwanza but nkasema huyu ndo wa kunipa majibu ya maswali yangu yote ngoja nifanye anavyotaka huku nikimchunguza ni nani anayemtuma.....

0 comments: