USAJILI ORODHA YA WALIOSAJILIWA NA WANAOTOKA SIMBA HADI SASA KWA MSIMU WA 2019/2020




WACHEZAJI WAPYA SIMBA SC
Katika kuimarisha kikosi chake simba imefanya usajili wa wachezaji kadhaa wa kimataifa ikiwemo wabrazil watatu.

Kennedy Wilson Juma
Ingizo jipya kwenye kikosi cha Mabingwa, beki wa kati Kennedy Wilson Juma amesaini mkataba wa miaka miwili. Uwepo wa Kennedy kwenye kikosi kwa kushirikiana na mabeki wengine tulionao ni hakika safu yetu ya ulinzi itakuwa imara zaidi. #NguvuMoja

GERSON FRAGA VIEIRA
Mchezaji mwingine kutoka Brazil mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira (26) amesaini mkataba wa miaka miwili na Mabingwa wa nchi. @g.fragav ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson, pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20 na alicheza klabu kadhaa za Brazil ikiwepo Grêmio amejiunga na klabu yetu akitokea ATK FC ya India. #NguvuMoja

Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman
Kiungo Bora mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu ya Sudan na mchezaji wa timu ya Taifa ya Sudan tangu akiwa na miaka 17 akitokea kwa mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya Sudan klabu ya Al Hilal, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman amejiunga na Mabingwa wa nchi kwa mkataba wa mwaka mmoja. Karibu Msimbazi Sharaf. #NguvuMoja

DEOGRATIUS KANDA
Kazi ya kusajili wakali watakaohakikisha kikosi cha Mabingwa kinazidi kuwa tishio kwa wapinzani inaendelea. Mshambuliaji raia wa Congo DR, Deo Kanda (29) amejiunga na Mabingwa wa nchi. Kanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Msimbazi akitokea TP Mazembe ambapo alikuwa mmoja wa wachezaji ambao waliiwezesha kushinda Ubingwa wa Afrika mwaka 2009, 2010 (aliifungia goli kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Esperance) na 2013 lakini pia akiwa ameshiriki Kombe la Dunia la Vilabu mwaka 2009, 2010, 2013. #NguvuMoja

Tairone Santos da Silva 
Kazi ya kuimarisha kikosi cha Mabingwa wa nchi inaendelea kama kawaida, beki Tairone Santos da Silva (30) amesaini mkataba wa miaka miwili kuchezea Msimbazi. @tairone89 amejiunga na klabu yetu akitokea ya Atlético Cearense FC ya nchini kwao Brazil. #NguvuMoja

Wilker Henrique da Silva
Mshambuliaji raia wa Brazil, Wilker Henrique da Silva akisaini mkataba wa miaka miwili kuchezea kikosi cha Mabingwa wa nchi. @wilkerhenrique95 mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na timu yetu akitokea klabu ya Bragantino ya nchini kwao Brazil. @wilkerhenrique95 karibu sana. Yajayo yatafurahisha zaidi. #NguvuMoja

IBRAHIM AJIB TETESI
GADIEL MICHAEL TETESI
FRANCIS KAHATA TETESI 
WALTER BWALYA TETESI

WANAOONDOKA
ASANTE KWASI - GHANA
NICOLAUS GYAN - GHANA
EMMANUEL OKWI - UGANDA
RASHID JUMA - TANZANIA MKOPO KMC
JAMES KOTEI - KAIZER CHIEFS FREE TRANSFER
HARUNA NIYONZIMA - FREE
DEOGRATIUS MUNISHI FREE



0 comments: